TANGAZO

TANGAZO

DKT. SAMIA : KIGOMA KUWA KITOVU CHA BIASHARA NA UCHUMI WA KIKANDA



Mgombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM Taifa amehitimisha duru ya kwanza ya kampeni ya kusaka kura za nafasi ya Urais katika mkoa wa Kigoma ambapo jana amefanya mkutano mkubwa wa hadhara katika jimbo laKigoma mjini. 

Dkt. Samia amelakiwa na mamia kwa maelfu ya wananchi wa wilaya ya Kigoma ujiji licha ya mkutano huo kufanyika asubuhi. 

Kupitia mkutano huo Dkt. Samia amenadi sera na mipango ya CCM katika kipindi cha miaka mitano ijayo ikiwa wananchi wa mkoa wa Kigoma watamchagua yeye na wagombea wengine wa nafasi ubunge na udiwani.

“Enzi za Kigoma kuitwa mwisho wa reli zimekwisha,” alisema Dkt. Samia akihutubia wananchi.

 “Kwa kasi ya maendeleo ya sasa, Kigoma inajengeka kuwa kitovu cha biashara na uchumi wa kikanda.” Alifafanua kuwa mradi wa reli ya kisasa (SGR) hauishii Kigoma pekee, bali unasonga mbele hadi Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. 

Alikumbusha ziara zake za mwaka 2022 katika maeneo ya Kakonko na Kibondo, ambapo alizindua barabara ya Kabingo–Nyakanazi, mradi wa maji na hospitali ya wilaya, akisisitiza kuwa kazi hiyo itaendelezwa. 

Mgombea wa Urais kupitia CCM Mhe. Dkt. Samia Suluhu Has Hassan amewaomba wananchi wa mji wa Kigoma kuiamini CCM katika uchaguzi mkuu ujao ili iendelea na dhamira yake ya kuifanya Kigoma kama kitovu cha uchukuzi.

 Mhe. Samia ameeleza kuwa uboreshaji wa uwanja wa ndege wa Kigoma unaendelea sambamba na kuimarishwa kwa shirika la ATCL. Mradi wa SGR kipande cha Tabora–Kigoma na Uvinza–Msongati (Burundi) unaendelea, huku vipande vya Dar es Salaam–Dodoma–Morogoro vikiwa vimekamilika.

 Katika hatua nyingine Mhe. Dkt. Samia ameeleza kuwa Serikali anayoiongoza imenunua vichwa vipya vitatu vya treni, mabehewa 22 ya 

abiria na 44 ya mizigo, na kufanya ukarabati wa mabehewa zaidi ya 350 ya mizigo na 33 ya abiria. 

Aidha, amewahakikishia wananchi kuwa serikali yake inaendelea kuboresha na kuendeleza bandari za Ujiji, Kibirizi na Kabwe. 

Kwa kuwa mkoa wa Kigoma unategemea usafiri wa majini CCM na serikali anayoiongoza inaendelea na Ujenzi wa meli nne katika Bandari ya Kalema ambapo moja imekamilika, tatu zipo hatua za mwisho sambamba na ukarabati wa meli kongwe. Vilevile, shipyard ya Katabe inaendelea na ujenzi wa meli mbili za mizigo, ikiwemo meli ya Ziwa Tanganyika yenye uwezo wa kubeba tani 3,500 ambayo itapokea shehena kutoka SGR. 



Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com