Mamia na maelfu ya wananchi wa manispaa ya Tabora siku ya jana tarehe12 Septemba 2025 wamejitokeza kwa wingi kumlaki na kumsikiliza mgombeawa Urais kupitia chama cha Mapinduzi CCM Dkt. Samia Suluhu Hassanakiendelea na kampeni zake mkoani Tabora.
TABORA NI KITOVU CHA HISTORIA YA NCHI YETU AMESEMA DKT. SAMIA
Mgombea wa Urais wa kupitia chama cha mapinduzi Dr.Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa Tabora kujivunia na kutambua kuwa mkoa wao ni kitovu cha historia ya nchi yetu. Dkt. Samia alisisitiza nafasi ya kipekee yaTabora katika historia ya kisiasa ya Tanzania.
Tabora ndipo aliposoma Baba na mwasisi wa Taifa letu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambapo pia alifanya kazi ya kufundisha Tabora. Mbali na hilo Mhe. Samia alisema Tabora inabeba alama isiyofutika ya maamuzi muhimu ya kihistoria yaliyofanyika mkoani hapo, ikiwemo ya kuwa mwenyeji wa mkutano mkuu wa TANU mwaka 1958 ulioamua kushiriki uchaguzi uliosogeza nchi karibu na uhuru. Aidha,alieleza kuwa mnara wa kumbukumbu uliopo Tabora hadi leo unabaki kuwa alama ya safari ya Tanzania kuelekea uhuru wa kisiasa. Dkt. Samia alisema kuwa baada ya kupatikana kwa uhuru wa kisiasa, taifa linaendeleza mapambano ya uhuru wa kujitegemea kiuchumi. Alisisitiza dhamira ya CCM ya kujenga taifa lenye uchumi jumuishi, linalozingatia ustawi wa wananchi wote.
Alinukuu kauli ya Mwalimu Nyerere kwamba maendeleo lazima yaletwe na watu wenyewe na yawafikie wananchi kule waliko,akibainisha kuwa serikali itahakikisha maendeleo jumuishi yanafika vijijini na mijini.
HUDUMA ZA KIJAMII
Akizungumzia sekta za kijamii na kiuchumi, alisema kuwa Tabora imepiga hatua kubwa katika elimu, afya, nishati, umeme, kilimo na maji, lakini bado mahitaji hayajatosheleza.
Aliahidi kuwa serikali ya CCM ikipata ridhaa itaendeleza miradi iliyopo na kuanzisha mipya, hususan katika afya, elimu, maji, kilimo, ufugaji na uvuvi.
VITONGOJI NA MAENEO YOTE YA TABORA KUFIKIWA NA UMEME ASISITIZA DKT. SAMIA
Mgombea wa Urais kupitia tiketi ya CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewaomba wananchi wa Manispaa ya Tabora kumchagua yeye kwa kishindo katika uchaguzi mkuu ili kukamilisha usambazaji wa huduma ya umeme katika manispaa ya Tabora.
Dkt. Samia ametoa ahadi ya kujenga kituo cha kupokea na kupooza umeme maeneo ya Urambo na Kaliua, ambayo hadi sasa ahadi hiyo imefanyiwa kazi na pia ahadi ya kuanzisha kituo cha kudhibiti mifumo ya usambazaji wa umeme maeneo ya Ziba, Wilaya ya Igunga.
TABORA KUKAMILISHWA MIRADI YA KIMKAKATI YA UCHUKUZI- DKT. SAMIA Wananchi wa manispaa ya Tabora mkoani Tabora wametakiwa kuendelea kumuunga mkono Mgombea wa Urais kupitia CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili aendeleze miradi ya sekta ya uchukuzi kwa mahusisi wake kukamilisha na kuboresha kiwanja cha ndege cha Tabora ambao umefikia asilimia 95 na tayari kimeanza kutumika.
Aidha, alieleza kuwa miradi mingine ya kimkakati inayogusa moja kwa moja Tabora, ni pamoja na bomba la mafuta kutoka Uganda kwenda Tanga linalopita Nzega na Igunga na mradi wa reli ya kati (SGR) kutoka
SGR
Tabora - Matukupora hadi Isaka alibainisha kuwa vituo vya vitakavyowekwa Tabora vitafungua fursa za ajira na biashara.
WAKULIMA TABORA KUNUFAIKA ZAIDI NA RUZUKU YA PEMBEJEO 2025-2030 –
DKT.SAMIA SULUHU HASSAN
Mkoa wa Tabora kwa sehemu kubwa Uchumi wake umebebwa na sekta kubwa ya Kilimo, kwa msingi huo chama cha Mapinduzi kupitia mgombea wake wa Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM
Taifa amewaomba wananchi wa Tabora kujitokeza kwa wingi siku ya tarahe 29 oktoba siku ya upigaji kura na kumchagua yeye na wagombea wengine wa chama cha Mapinduzi ili kuendeleza miradi ya maendeleo kwenye sekta muhimu za uzalishaji mkoani humo ikiwemo sekta ya kilimo.
Ambapo ameahidikuendelea kutoa ruzuku za mbolea, pembejeo sambamba na kuendelea kuongeza na kuboresha eneo la skimu za umwagiliaji ili wakulima wazalishe
mara mbili kwa mwaka, kwa kujibu wa ilani ya CCM ya 2025-2030 kitaifa CCM inalenga kuongeza eneo la umwagiliaji kutoka 983,466.06 za sasa hadi milioni 5 katika kipindi cha mwaka 2025-2030.
WAFUGAJI TABORA KUNUFAIKA HUDUMA ZA CHANJO, MAJOSHO -AMESEMA
DKT. SAMIA
Dkt. Samia ameahidi kupaisha wafugaji wa wilaya ya Tabora. Mgombea wa Urais kupitia chama cha Mapnduzi Dkt. Samia Suluhu Hassan ameahidi kuendelea kuinua wafugaji wa wilaya ya Tabora ikiwa watampatia ridhaa ya kuwaongoza tena katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu kwa kuwa atajenga na kuboresha chanjo, kuboresha minada na kuongeza majosho ili kuongeza tija kwa wafuagaji.
TABORA KUWA NA UHAKIKA WA MAJI- MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN Changamoto za Maji kumalizika katika mkoa wa Tabora kipindi cha 2025-2030 asema Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Huku akiwaomba wananchi kumchagua yeye na wagombea wengine katika uchaguzi mkuu ujao ili ikamilishe miradi ya maji, Dkt. amesema miradi ya maji inaendelea kutekelezwa, ambapo utekelezaji umefikia asilimia 67 katika Wilaya ya
Sikonge.
Aliongeza kuwa mradi mkubwa wa maji kutoka Ziwa Viktoria utamaliza tatizo la upatikanaji wa maji katika mkoa mzima.
DKT. SAMIA KUKAMILISHA MIUNDOMBINU MBALIMBALI TABORA Mgombea wa Urais kupitia CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaomba wananchi wa Tabora kumchagua katika uchaguzi mkuu ujao ili kuukamilisha na kuboresha miradi ya miundombinu mbalimbali katika mkoa wote wa Tabora. Dkt amesema serikali yake katika miaka minne imeimarisha TARURA na kuongeza bajeti ya ujenzi wa barabara.
Amewaomba kukiunga mkono CCM na wagombea wake ili kujenga barabara ya mzunguko (ring road)yenye urefu wa kilomita 82 ili kupunguza msongamano wa malori katikati ya manispaa ya Tabora.
Aidha, alisema ndani ya mkoa wa Tabora serikali itajenga madaraja 132 katika barabara zilizoorodheshwa kwenye ilani na kuweka taa 2,300 za barabarani,hatua itakayowezesha Tabora kuwa jiji linalofanya biashara saa 24.
