TANGAZO

TANGAZO

DKT. SAMIA : TUTAPIMA ARDHI MTWARA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI KATI YA WAKULIMA NA WAFUGAJI


Tutapima Ardhi ya Mtwara Kumaliza Migogoro ya Ardhi Kati ya Wakulima na Wafugaji maneno ya Dkt Samia mgombea Urais CCM. 

Ahadi ya CCM kupitia mgombea wake wa urais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewaomba wananchi wa mkoa wa Mtwara kuwachagua yeye pamoja na wagombea wa chama hicho ili serikali iendelee kutatua changamoto ya migogoro kati ya wakulima na wafugaji. Akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika katika manispaa ya Mtwara Mikindani, Dkt. Samia amesema serikali ya CCM ikipewa ridhaa itapima na kupanga ardhi kwa mpangilio maalum ili kuondoa kabisa migongano inayojitokeza baina ya pande hizo mbili. 

Sambamba na hilo, ameahidi kuwa serikali itaongeza eneo la ufugaji kutoka hekta milioni 3 za sasa hadi kufikia hekta milioni 6 ifikapo mwaka 2030, hatua ambayo inalenga kutoa nafasi zaidi kwa wafugaji na kupunguza mivutano katika matumizi ya ardhi. 

Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com