TANGAZO

TANGAZO

KAMPENI YA KIJIJI KWA KIJIJI YA ADO SHAIBU YAFIKIA VIJIJI 40



Mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini kwa tiketi ya ACT Wazalendo Ndugu Ado Shaibu Ado amevifikia vijiji 40 vya Jimbo hilo kupitia kampeni yake ya Kijiji kwa Kijiji ambayo sasa imefikia siku ya 12 tangu uzinduzi wa kampeni yake tarehe 7 Septemba 2025.

Vijiji hivyo vinapatikana katika Kata 12 kati ya Kata 24 za Jimbo la Tunduru Kaskazini. Kata zilizotembelewa ni Majimaji, Muhuwesi, Ngapa, Tinginya, Nampungu, Kidodoma, Nandembo, Matemanga, Namwinyu, Kalulu, Jakika na Ligunga. 

Kwenye ziara hiyo Ndugu Ado amebainisha kuwa vipaumbele vyake ni kutetea maslahi ya wakulima kwa kuondosha changamoto za mfumo wa stakabadhi ghalani, kuiwajibisha serikali kwenye udhibiti wa tembo, kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za kijamii hasa maji, barabara za vijijini, madarasa na usambazaji wa nguzo za umeme vijijini na utetezi wa haki za wananchi wa Tunduru bila kujali itikadi za kivyama.

Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com