Chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, Bajeti Kuu ya Tanzania iliongezeka kutoka shilingi trilioni 36.23 ( dola bilioni 15.10) hadi trilioni 41.48 ( dola bilioni 17.28), ikiwa ni ongezeko la asilimia 14.5, sawa na shilingi trilioni 5.25.
Ongezeko hili liliongeza pia bajeti ya kilimo kutoka shilingi bilioni 294.2 hadi bilioni 751.1, bajeti ya afya kutoka trilioni 1.2 hadi trilioni 1.4.
Kitendo cha Rais Samia kuongeza bajeti kwenye sekta hizi zinazochochea uchumi kunalenga kumpa kila Mtanzania maisha bora na furaha kwenye nchi yake.
