"Tunataka mfugaji anenepe na ng'ombe ananepe" Ni Kauli ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inayodhihirisha dhamira yake ya kuboresha sekta ya mifugo nchini, Katika kipindi chake cha kwanza cha uongozi, Rais Samia ametambua kuwa sekta ya mifugo ni moja ya nguzo muhimu za uchumi wa taifa, ikiajiri idadi kubwa ya Watanzania. Hata hivyo, sekta hii kwa muda mrefu imekuwa ikikabiliwa na changamoto za ukosefu wa tija, hali iliyosababisha wafugaji kushindwa kunufaika ipasavyo kutokana na uduni wa mifugo.
Katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake, hatua kadhaa zimechukuliwa kuboresha sekta hil. Miongoni mwa hatua hizo ni kuanzishwa kwa programu ya Chanjo ya Taifa ya mifugo yenye thamani ya sh.bilioni 216 iliyolenga kupunguza vifo vya mifugo. Jitihada hizi za Mhe.
Dkt. Samia Suluhu Hassan zimepelekea kupungua kwa vifo vya mifugo kutoka 27 kwa kila mifugo hai 100 mwaka 2020 hadi 12 kwa kila mifuga hai 100 mwaka 2024. Aidha, uzalishaji wa nyama umeongezeka kutoka tani 702,000 mwaka 2020 hadi tani 803,264 mwaka 2024, huku uzalishaji wa maziwa ukipanda kutoka lita bilioni 3.01 mwaka 2020 hadi lita bilioni 3,97 mwaka 2024. Kuongezeka kwa uzalishaji wa nyama kufikia tani 1,054,114.03 zenye thamani ya shilingi trilioni 10.38 mwaka 2025, na mauzo ya nyama nje ya nchi kufikia dola za Marekani milioni 61.4, sawa na ongezeko la asilimia 780. Ongezeko hili mauzo imechagizwa na ongezeka la viwanda vya kuchakata nyama kutoka 3 mwaka 2021 hadi 7 mwaka 2025. Aidha ameongeza eneo malisho kutoka hekta 700,799 hadi hekta milioni 3.49 kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa katika awamu zote.
Sekta ya mifugo ni ajenda endelevu kwa Rais Samia, ambapo ameahidi kutenga na kupima maeneo ya ufugaji kutoka hekta 3,466,111.43 hadi hekta 6,000,000 katika kipindi cha mwaka 2025-2030. Mpango huu utasaidia kuongeza huduma muhimu kama maji, majosho, malisho na huduma za ugani, hatua itakayowezesha wafugaji kunufaika zaidi.