Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan imejenga na kukarabati kipande cha barabara cha kutoka Kigamboni– Kibada chenye urefu wa kilometa 4.8 kwa gharama ya takribani Shilingi bilioni 8.7, kikitoa jumla ya makisio ya ajira 860 zikiwemo makisio ya ajira 280 za moja kwa moja na makisio ya ajira 580 za muda.
Mradi huu utanufaisha wakazi wa Kigamboni, Kibada, Kijichi na Mjimwema, ukiwa chachu ya kurahisisha usafiri na kukuza shughuli za kiuchumi katika maeneo ya Kigamboni na jiji zima la Dar es Salaam