Chini ya Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, Tanzania imejenga meli kubwa ya kisasa ya MV Mwanza “Hapa Kazi Tu” inayofanya kazi katika Ziwa Victoria.
Meli hii ina uwezo wa kubeba abiria 1,200, mizigo tani 400, magari madogo 20 na magari makubwa 3 kwa mpigo. Ina muundo wa ghorofa 4 na uzito wa tani 3,500.
Ujenzi wa meli hii umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 109, na umechangia kutoa ajira za moja kwa moja zaidi ya 300 pamoja na ajira zisizo za moja kwa moja zaidi ya 1,000.
Mbali na mchango wake katika ajira, meli hii inatarajiwa kuchochea ukuaji wa uchumi mkubwa, jumuishi na wa kisasa, na hivyo kuifanya Tanzania kuwa kinara miongoni mwa nchi za maziwa makuu katika biashara na Uchumi wa Bluu.
