TANGAZO

TANGAZO

CHINI YA UONGOZI WA DKT. SAMIA UJENZI WA STENDI YA KISASA YA MABASI MOROGORO YAZINDULIWA

Chini ya Rais Samia, Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro imezindua ujenzi wa stendi ya kisasa ya mabasi ikiwa karibu na Stesheni ya SGR ya Jakaya Kikwete, kwa gharama ya shilingi bilioni 13.4 kupitia mpango wa TACTIC (Tanzania Cities Transforming Infrastructure and Competitiveness),mradi unatarajiwa kukamilika ifikapo Julai 21, 2026.

Stendi hii itakuwa na hoteli yenye vyumba 30, mgahawa na sehemu ya burudani, kumbi za mikutano, maduka 18 ya ukubwa tofauti, ofisi 11 za kupangisha, vibanda vya kisasa vya mama/baba lishe, kituo cha polisi, vyoo vya kisasa, kituo cha ulinzi, maeneo ya maegesho kwa mabasi, bodaboda na bajaji, pamoja na sehemu 15 za kungoja abiria.

 Vilevile, barabara mbili zenye lami zenye urefu wa kilomita moja kila moja zitajengwa kuunganisha eneo hilo, na daraja kubwa litajengwa ili kuunganisha moja kwa moja stendi na stesheni ya SGR, hatua ambayo inalenga kuboresha huduma za usafiri, kurahisisha safari za abiria wa ndani na nje ya Morogoro, kuongeza ajira na fursa za biashara, na kuifanya Morogoro kuwa kitovu cha usafiri mchanganyiko kati ya reli ya kisasa na mabasi.


Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com