Na. Mwandishi wetu
Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, tunawaomba Watanzania wote kutambua ukweli mmoja muhimu: Misingi imara ya Sayansi, Teknolojia, na Ubunifu (STI) tayari imewekwa. Kura zetu sasa zinapaswa kuelekezwa katika kuhakikisha kunakuwa na mwendelezo thabiti ili kufikia malengo ya Tanzania kuwa kitovu cha Kidigitali Afrika Mashariki.
Serikali ya sasa imesisitiza wazi kwamba sayansi na teknolojia ni nguzo kuu ya uchumi wa kisasa. Hii si ahadi tu, bali ni utekelezaji unaoonekana kwenye Ilani ya Chama Tawala (CCM) na matendo ya Serikali.
Kura Yako Ihakikishe Mwendelezo
Kazi kubwa imefanyika katika kuanzisha vituo atamizi (Innovation Hubs), kuendeleza sera za Akili Bandia (AI), na kuleta uwazi wa kidigitali katika huduma za Serikali (asilimia 50 ya huduma kutolewa kidigitali).
Misingi Ilishawekwa, Tunahitaji Jengo la Kudumu:
Wakati wa kampeni, kuna vyama na wagombea wengi wanaoweza kuahidi 'mapinduzi' mapya. Lakini kwa sasa, Tanzania haihitaji kuanza upya; inahitaji kujenga juu ya misingi iliyopo!
Kama unataka kuona:
Ajira zaidi katika uhandisi wa kielektroni na Ujasiriamali wa TEHAMA.
Ufanisi zaidi katika huduma za Serikali.
Tanzania ikiwa kiongozi wa uchumi wa kidigitali Afrika Mashariki.
Basi, kura yako ya Oktoba 29 inapaswa kuelekezwa kwa mgombea na chama chenye uwezo na dhamira ya kuendeleza na kukuza yale yote mema yaliyojengwa, badala ya kuanzisha safari mpya yenye mashaka.
