TANGAZO

TANGAZO

TASACO YAFANIKIWA KUWAWEZESHA WATOTO WENYE UHITAJI KWA KUWAPA MAHITAJI MAALUM


Taasisi isiyo ya kiserikali ya Tanzania Samaritan Community Organization (TASACO) Imefanikiwa kuwawezesha Jumla ya watoto 50 wenye uhitaji kupata Elimu bora kwa kuwapatia vifaa vya shule na fedha, 48 ni wanafunzi wa shule ya Msingi na Wawili wanasoma shule ya upili.


Ameyazungumza hayo Oktoba 14,2025 Kwenye Mkutano Mkuu wa TASACO uliofanyika kwenye Viwanja vya Mako Makuu ya Taasisi hiyo iliyopo Ilala Jijini Dar es salaam ,Mkurugenzi Paul Chegere amesema kuwa Mradi wao wa Somesha Mtoto mmoja ni kuwasomesha watoto hao ili kuwawezesha kutimiza ndoto zao za kufanikiwa.



Chegere amesema kuwa moja ya faida ya Mradi huo ni kutengeneza kizazi chenye utu na kitakachoweza kusaidia kuondoa umasikini na kuletwa Maendeleo yenye tija kwa Taifa.

Mkutano Mkuu huo umefanyika ili kufanya tathmini ya Miradi ambayo imefanyika kwa mwaka uliopita,Mkurugenzi Chegere Ameitaja Miradi Miwili itayokwenda kufanyika kwa mwaka 2025 /2026 ambayo ni Bemefo utakaojumuisha Malezi,Afya ya Akili na Elimu bora,Huku Mradi wa pili ni CMG Goldstone utakaojumuisha Maisha bora,mitaji endelevu na makazi.

TASACO ni Taasisi isiyo ya Kiserikali iliyoanzishwa na kusajiliwa February 28,2025 yenye maono ya kuifikia Jamii ya wajasiriamali WA kipato Cha CHINI,Kati na juu na wote kwa pamoja kufanikiwa KATIKA maisha.

Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com