TANGAZO

TANGAZO

WASHIRIKI MNADA WA PIKU KUJIPATIA SAFARI ZA BOLT ZENYE THAMANI YA SH. 100, 000

 


Jukwaa la kidijitali linaloendesha minada ya kipekee mitandaoni la Piku Africa limezindua bidhaa yake mpya itakayopatikana katika Combo la Piku ambayo itawapa washiriki nafasi ya kujishindia koponi yenye thamani ya Sh. 100,000 kwa matumizi ya kila siku ya usafiri kupitia Bolt.


Akizungumza kuhusu fursa hiyo, Meneja Uendeshaji wa Biashara Piku, Sia Melewas amesema kuwa koponi hiyo ni maalum kwa wafanyabiashara na wananchi wa kawaida kabisa wanaotaka kurahisisha shughuli zao za kila siku kwa kupitia usafiri.

Amesema kupitia combo hilo la Piku mtu anaweza kujipatia safari za Bolt zenye thamani ya Sh. 100,000 hivyo amewataka watu kuchangamkia fursa hiyo ya kipekee yenye lengo la kuendelea kuwarahisishia wateja wao huduma.

“Vijana, wanawake kwa wanaume tunawakaribisha kuanza sasa kuingia katika mnada wetu huu ili kuweza kujipatia koponi hiyo na bidhaa zingine zingi, washiriki wote kuanzia umri wa miaka 18 wanakaribishwa kushiriki kwa kupakua App ya Piku kupitia Play Store (kwa watumiaji wa Android) au App Store (kwa watumiaji wa iPhone).

“Tiketi za ushiriki zinapatikana kwa bei nafuu; Sh. 1,000 kwa tiketi 10, Sh. 5,000 kwa tiketi 50, na Sh. 100,000 kwa tiketi 100. Kadri unavyoongeza tiketi, ndivyo nafasi ya kushinda inavyoongezeka,” amesema Melewas

Hata hivyo Melewas amesema kuwa jukwaa hilo la Piku limepanga kumaliza mwaka 2025 kwa kishindo, ambapo mshindi mmoja atajinyakulia gari aina ya Toyota Raum, lenye bima ya mwaka mzima na kadi ya mafuta, vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Sh. milioni 30.

Aidha, mwanzoni mwa Desemba mwaka huu, “Mgodi wa Piku” utatoa zawadi ya seti ya dhahabu safi yenye thamani ya Sh. milioni 6, ambapo mshindi atapata uhuru wa kuchagua seti anayoitaka dukani.

Vilevile, kila baada ya siku tatu, mshiriki anaweza kujishindia simu janja aina ya Samsung A06 yenye thamani ya Sh. 250,000, huku baada ya siku 28, kupitia “Zigo la Piku”, mshindi atakayetoa dau dogo na la kipekee ataondoka na pikipiki mpya aina ya TVS yenye helmet, reflector, bima, na kadi ya mafuta ya miezi sita, vyote vikiwa na thamani ya Sh. milioni 4.

Kwa upande mwingine, Melewas amesema kila baada ya siku 14, kupitia Combo la Piku, washiriki wana nafasi ya kushinda saa ya kisasa, manukato ya kifahari, televisheni ya LG inchi 55 na Airtel Router iliyolipiwa mwaka mzima, zenye jumla ya thamani ya Sh. milioni 2.4.



Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com