TANGAZO

TANGAZO

NAIBU WAZIRI KISUO : OSHA ELIMISHENI WAFANYABIASHARA WADOGO




Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Rahma Kisuo ameitaka Menejimenti ya Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kuhakikisha programu za kutoa elimu kwa Wajasiriamali wanaofanya biashara ndogo ndogo zinakuwa endelevu ili kuwajengea uelewa wa vihatarishi vilivyopo katika shughuli wanazozifanya.



Mhe. Kisuo amebainisha hayo leo Desemba 8, 2025 Jijini Dar es salaam wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo kuhusu Usalama na Afya kwa Wajasiriamali hao.

Amesema, Wajasiriamali ni kundi muhimu linalochangia kwa kiasi kikubwa uchumi wa Taifa, hivyo ni muhimu kuwapatia mafunzo ili waweze kutekeleza shughuli zao bila kuhatarisha maisha yao.

Aidha, amesisitiza kuwa mafunzo hayo yatasaidia kupunguza ajali, magonjwa yatokanayo na kazi pamoja na kuongeza tija katika uzalishaji, hivyo ni muhimu kubuni programu za mafunzo kwa makundi mbalimbali ya wafanyabiashara ndogo ndogo kwa sekta zote hapa nchini.

Sambamba na hayo, ametoa wito kwa wafanyabiashara hao kutojihusisha na makundi yenye nia ya kuvuruga shughuli za uzalishaji na kuvunja amani ya nchi ya Tanzania. 

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa OSHA Khadija Mwenda, amesema wataendelea kutoa elimu hususan kwa vijana wanaojikita katika biashara ndogo ndogo ili watambue umuhimu wa kutumia vifaa kinga katika shughuli zao za kila siku ikiwa ni pamoja na kuzingatia taratibu nyingine za kujilinda na madhara yatokanayo na kazi.

Akizungumza mmoja wa Wajariamali walioshiriki katika ufunguzi wa Mafunzo hayo Jesca Charles, wameishukuru OSHA kwa kuwapatia elimu na vifaa kinga ambavyo vitawasaidia katika kazi zao za kila siku.



Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com