TANGAZO

TANGAZO

NGORONGORO YAWEZESHA VIKUNDI VYA KINAMAMA KUFANYA ZIARA YA MAFUNZO NDANI YA HIFADHI



Na. Mwandishi wetu, Ngorongoro

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii imewawezesha  wakinamama 84 kutoka Kata ya Ganako, wilayani Karatu, kufanya ziara ya mafunzo ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro baada ya kupewa mafunzo ya kutengeneza majiko banifu ili kulinda mazingira.



Ziara hiyo ni sehemu ya programu ya elimu kwa vitendo inayolenga kuhamasisha uhifadhi wa mazingira na matumizi ya teknolojia rafiki na kuepuka kukata miti na matumizi ya mkaa kwa jamii inayozunguka hifadhi ya Ngorongoro.

Akizungumza katika ziara hiyo, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Bi. Lightness Kyambile, amesema hatua hiyo inalenga kuwawezesha wanawake kuwa mabalozi wa uhifadhi katika jamii zao ili kuepuka kukata miti, kuchoma mkaa na kuharibu mazingira.

Akina mama walioshiriki ziara hiyo wametoa shukrani kwa uongozi wa Ngorongoro kwa kuwapa nafasi ya kujifunza kwa vitendo na kuahidi  kuendelea kutoa  elimu hiyo kwa wanawake wengine katika vijiji vyao.

Ziara hiyo ya mafunzo  imeandaliwa  kwa kuwashirikisha Ganako Youth, ambao wamekuwa mstari wa mbele kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira na kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala.






Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com