TANGAZO

TANGAZO

MJUMBE WA MKUTANO MKUU MKOA JANETH MWAMBIJE ASHIRIKI KWENYE KIKAO CHA DIWANI WA KATA YA KIVULE



Mjumbe wa mkutano mkuu mkoa (DSM), Ndg. Janeth Thomson Mwambije, ameshiriki kikamilifu kwenye kikao cha mheshimiwa diwani wa kata ya Kivule. Mhe. Rajabu Omari Manyinya, kama mdau wa Elimu kwenye kata hiyo.

Katika kikao hicho, Bi. Janeth Thomson Mwambije alipata wasaa wa kuwasilisha mawazo yake, ambayo ni;

Kuanzisha mtihani wa mjumbe wa mkoa, ambao utakuwa unafanyika kwa madarasa ya mitihani yaani kidato cha pili, cha nne, na cha sita itapoanza rasmi. Ili iwe sehemu ya kuwasaidia wanafunzi kujua mbinu za maswali na namna nzuri ya kujibu maswali. Lakini pia, kuwa hamasa ya wanafunzi kujisomea mara kwa mara. 

Lakini pia, Ili Kuomba ushirikiano wa wafanyabiashara wa maduka kuuza taulo za kike kwa pisi moja moja kwa shilingi mia tatu (300/=Tshs) ili kuwasaidia wanafunzi waishio kwenye mazingira magumu kumudu gharama za taulo za kike huku wakitafuta suluhu ya kudumu ya changamoto hiyo. Akiwaomba kuwa kwa wao kuridhia hilo watakuwa wameigusa jamii kama wajenzi chanya wa taifa la Tanzania.

Malengo hayo yenye mlengo wa kuboresha maisha ya wanafunzi wa shule hizo za serikali za kata ya Kivule, ambazo ni Misitu, Kerezange, Kivule, Kumbilamoto (Mpya), Na Abuuy Jumaa, zinalenga kuhakikisha ifikapo 2030 waweze kuondoa daraja sifuri na daraja la nne, katika shule hizo.

Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com