TANGAZO

TANGAZO

SHAROBARO WA NYUMBU NDANI YA NDUTU





Sharobaro  wa Nyumbu  au kijana wa nyumbu anayezaliwa Ndutu ni tofauti na vijana binadamu wanaozaliwa mijini kama  Dar es Salaam



Nyumbu wana mpangilio wa kushika mimba na kuzaliwa kwa pamoja kitaalumu (Synchronization.) Hii ni moja ya maajabu makubwa ya nyumbu wanaopatikana Hifadhi ya Ngorongoro  na wanaokamilisha ikolojia ya Nyumbu katika mfumo wa Serengeti.

Ndama wa nyumbu ni wa kipekee, ndani ya dakika chache tu baada ya kuzaliwa, tayari anakuwa na uwezo wa kusimama na kukimbia huku akianza kujitegemea.

Katika kudhihirisha kuwa titi la mama ni tamu sharobaro wa nyumbu pamoja na kuzaliwa wengi lakini hakuna ndama atakayenyonya titi la mama si wake ingawa jukumu la ulinzi ni la jamii yote hii ni kudhihirisha mtoto wa mwenzio ni wako.

Mtoto wa nyumbu akitimiza miezi sita mpaka kumi na mbili anaanza kupiga michongo ya masafa marefu Kama walivyo wangoni na wasumbwa ambao kutembea masafa kwao si shida.

Pamoja na mnyama Nyumbu kudharaulika lakini ni mwepesi wa kujitegemea tofauti kabisa na baadhi ya mashorobaro wa mjini ambao hadi wanazeeka hutegemea wazazi kwa chakula, malazi, mavazi na mengineyo.

Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com