TANGAZO

TANGAZO

WATOA HUDUMA YA LPG PWANI WAKUMBUSHWA USALAMA





Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Mashariki imewakumbusha wafanyabiashara na wadau wa gesi ya kupikia (LPG) kuzingatia usalama, afya na utunzaji wa mazingira, wakati wa kusafirisha, kuhifadhi na kuuza bidhaa hizo kwa wateja.




Meneja wa EWURA Kanda ya Mashariki, Mha. Lorivii Long’idu, akizungumza wakati wa semina ya wadau hao iliyofanyika mkoani Pwani,  24 Februari 2026 aliwasisitiza wafanyabiashara wa jumla wa LPG kuwa na mikataba na wasambazaji  wao na wauzaji wa rejareja wa bidhaa hiyo ili kukidhi matakwa ya kisheria na kiusalama.


Mha. Long’idu aliwahimiza pia wadau hao kuwaelimisha  wasambazji na wauzaji wa rejareja wa LPG  kuhusu usalama na umuhimu wa kutumka mizani iliyohakikiwa na Wakala

wa Vipimo wakati wa kutoa huduma ili wananchi wapate huduma bora.

Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com