TANGAZO

TANGAZO

WAZIRI KABUDI AKUTANA NA MJUMBE MAALUM WA KATIBU MKUU WA JUMUIYA YA MADOLA



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Mhe.  Prof. Palamagamba Kabudi amekutana na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Mhe. Lazarus Chakwera jijini Dar Es Salaam Aprili 09, 2026.


Mjumbe Maalum huyo yupo nchini kwa ziara ya kikazi ambapo atakutana na wadau mbalimbali jijini Dar Es Salaam, Dodoma na Zanzibar.

Wakati wa ziara hiyo ambayo itahimishwa Aprili 16, 2026. Mhe. Chakwera amepangiwa miadi ya kukutana na viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, asasi za kiraia na viongozi wastaafu.

Mhe. Chakwera aliwasili nchini Aprili 08, 2026 na kupokelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe na alianza ratiba yake kwa kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo Aprili 09, 2026 jijini Dar EsSalaam.




Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com