TANGAZO

TANGAZO

WATUHUMIWA WANNE WAKAMATWA MAUAJI YA JAMES TEMBA WA IFM

 




Taarifa ya Jeshi la Polisi kuhusu KIFO cha James Temba Mwanafunzi wa Mwaka wa Pili Chuo cha IFM👇

Jeshi la Polisi Kanda Maalum  Dar es Salaam linaendelea kupeleleza kwa uzito mkubwa tukio la  mauaji ya  ya mtu aliyetambulika  kwa jina la James Rogers  Temba mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo cha IFM Dar es Salaam ambaye mwili wake ulikutwa unaelea kwenye maji yaliyokuwa yanatiririka katika mto Msimbazi eneo la Kipawa Ilala tarehe 30.4.2026 huku  ukiwa hauna  kichwa. 

Polisi Dar es Salaam imewakamata watuhumiwa wanne ambao ni  1.Steven Rogers Chaka, Mmbugu miaka 31, Afisa maabara  Mkazi wa Bomang’ombe Hai Kilimanjaro 2. Anna Frank Lema @happines, Mchaga, miaka 30, mfanyabiashara Mkazi wa Tabata Chang’ombe 3. Twalibu Khamis @mputo  miaka 23 mkazi wa Kigogo Kati 4. Michael John @tambali miaka 26 mkazi wa Kigogo Kati. 

Vipo  pia baadhi ya vielelezo ambavyo vinachunguzwa kuhusiana na tukio hilo.Wito wa Jeshi la Polisi kwa wananhi ni kuwa watulivu ili kila aliyehusika kulingana na ushahidi aweze kuchukuliwa hatua za kisheria.  

Imetolewa na; Kamanda Kanda Maalum ya Polisi  Dar es Salaam