TANGAZO

TANGAZO

MKIIHESHIMU KAZI YENU NA WENGINE WATAIHESHIMU

 


Wasafirishaji wa abiria kwa kutumia Pikipiki maarufu kama Bodaboda Kijiwe cha Mkwajuni Kati wametakiwa kuijali na kuithamini kazi yao kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kutokubeba magendo na kusafirisha wahalifu, pia kutambua kuwa pikipiki ni chombo kinachobeba abiria mmoja na sio zaidi ya uwezo wa chombo hicho kwani kitendo hicho kinaweza kuhatarisha maisha yao.


Hayo yalisemwa Januari 16, 2025 na Polisi wa Kata ya Mkwajuni Wilaya na Mkoa wa Songwe Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Stella Rwekamwa wakati alipokuwa akitoa elimu juu ya kukipa kitu thamani (Branding) ili kiweze kuthaminiwa na wengine ikiwa ni pamoja na umuhimu wa kufuata na kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kupunguza na kuepuka ajari zinazoweza kuepukika katika kata hiyo.





Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com