Katika kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo kitaifa itafanyika Mkoani Arusha mtandao wa Polisi wanawake Arusha umeeleza ulivyojipanga kuimarisha ulinzi, kutoa elimu na kutembelea vituo vya wahitaji pamoja na kuunga Juhudi za Mheshimiwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutangaza vivutio vya utalii hapa nchini.
Akitoa taarifa hiyo afisa mnadhimu namba moja Mkoa wa Arusha ambaye pia ni mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi wanawake Mkoa wa Arusha Kamishina msaidizi wa Polisi ACP Debora Lukololo, amesema kuwa askari wa kike Mkoa wa Arusha kwa kishirikiana na askari wa kike mikoa mingine wamejipanga kuimarisha ulinzi kabla na baada ya shereke za maazimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo shamrashamra zake zitaanza Machi 01,2025 hadi 08 Mkoani humo.
Ameongeza kuwa maadhimisho hayo yataenda sambamba na utoaji wa elimu, misaada mbalimbali na kutembelea hifadhi za taifa ambapo amewaomba wageni na washiriki wengine kutambua kuwa mtandao wa Polisi wanawake umejipanga vyema kuimarisha ulinzi na Usalama wakati wote wa maadhimisho hayo.
ACP Lukololo amebainisha kuwa katika maadhisho hayo litakuwepo banda maalum la Polisi ambalo litakuwa na wataalamu mbalimbali wa Jeshi hilo watakaosililiza na kutakua changamoto za wananchi huku akitumia fulsa hiyo kuwaomba wananchi wenye changamoto katika masuala ya utalii kufika katika kituo Cha Polisi Cha Diplomasia na Utalii ambacho kinahusika na maswala yote ya Diplomasia na Utalii.
Kwa upande wake Mkuu wa Kikosi cha usalama Barabarani Mkoa wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Zauda Mohamed akaweka Wazi mikakati ya Kikosi cha usalama Barabarani kuelekea maadhimisho hayo ya siku ya wanawake duniani ambapo amesema kuwa wamejipanga vyema kuimarisha usalama Barabarani na kutoa elimu kupitia Banda maaalum ambalo litakuwepo katika maadhimisho hayo.
Mkuu wa dawati la Jinsia na watoto Mkoa wa Arusha Mrakibu wa Polisi SP Happness Temu akabainisha kuwa watatumia fursa hiyo ya siku ya wanawake duniania kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kusiana na vitendo vya kikatili vinavyofanywa na baadhi ya wanawake na wanaume katika jamii.
Kaimu Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha wao wakatumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutatua uhalifu huku Mkuu huyo wa Polisi Wilaya akisisitiza kuwa wamejipanga vyema kuimarisha ulinzi katika maadhimisho hayo.
