TANGAZO

TANGAZO

SMZ ITAENDELEA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI KWA WAWEKEZAJI - RAIS MWINYI


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi  amebainisha kuwa Serikali itaendelea kuweka Mazingira Wezeshi kwa Wawekezaji ili  kuongeza Idadi ya   Wawekezaji kwa kuimarisha huduma ikiwemo Ujenzi wa Viwanja vya Ndege, Barabara,Miundombinu ya Maji, Umeme na Afya.


Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo  baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Hoteli ya SANDIES NUNGWI BEACH RESORT ya Nungwi ,Mkoa wa Kaskazini Unguja.


Aidha Rais Dkt.Mwinyi ameziagiza Taasisi, Wadau na  Wananchi  kuendelea  kushajihisha Uwekezaji katika Sekta ya Utalii ili Zanzibar inufaike  zaidi na Mapato yanayotokana na sekta hiyo.


Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa  Uchumi wa Zanzibar umekuwa kwa asilimia 7.5  kunakochangiwa kwa kiasi kikubwa na Sekta ya Utalii .

Vilevile Rais Dkt.Mwinyi amezitaja Faida  kuu za Uwekezaji hapa nchini kuwa ni Ukuaji wa Uchumi, Ongezeko la Watalii ,Ongezeko la Kodi  na Upatikanaji wa fursa za Ajira hususan kwa Vijana.


Rais Dkt.Mwinyi ameipongeza Mamlaka ya Uwekezaji  ya Zanzibar (ZIPA) kwa kupunguza Muda wa Upatikanaji wa  Vibali vya Uwekezaji.


Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi ametoa rai kwa Wawekezaji wote kuhakikisha  Miradi yao Inawanufaisha Wananchi kwa  kuondoa  Matatizo   yaliomo ndani ya jamii ikwemo Ukosefu wa huduma za Maji Afya,Umeme na  Elimu.


Hoteli ya Sandies Nungwi Beach Resort inayomilikiwa na Kampuni ya Away Hotels Zanzibar Limited kwa asilimia 99 na Paolo Ross raia wa Itali kwa asilimia  itagharimu Dolla Milioni 17 hadi kukamilika Kwake ina vyumba 126 na kutoa fursa za Ajira 200.

Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com