TANGAZO

TANGAZO

MAMA MZAZI WA HAYATI MAGUFULI AFARIKI DUNIA



Mama Mzazi wa Hayati John Pombe Magufuli, aliyekuwa Rais Wa  Awamu ya Tano, Suzana Magufuli, amefariki dunia mjini Chato mkoani Geita baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Taarifa za kifo hicho zimethibitishwa na mtoto wa Hayati Magufuli, Jesca Magufuli, aliyesema kuwa Bibi Suzana amefariki nyumbani kwake Chato na kwamba familia itaendelea kutoa taarifa kuhusu taratibu za msiba huo.