TANGAZO

TANGAZO

ASKARI WA TAWA WAMUOKOA MNYAMAPORI ALIYETELEKEZWA NA WAZAZI WAKE



-Uhifadhi ni pamoja na kutoa huduma kwa wanyama wanaokutwa na changamoto mbalimbali. 

Katika picha hapo juu ni ndama wa mnyamapori aitwaye TANDALA ambaye aliokotwa na kikosi cha doria cha Askari wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA katika Pori la Akiba Kizigo Mkoani Singida akiwa hajiwezi kabisa. 

Kwa taarifa za kikosi inaonekana alizaliwa akatelekezwa na kundi. Ishara inayothibitisha hilo ni kitovu chake kukukutwa bado kibichi..

Askari hao walimhudumia Kwa kumpatia uji kwa siku tatu na baada ya kupata nguvu walimpeleka katika Ofisi za Pori la Akiba Kizigo Kwa huduma zaidi.

Kwa sasa anaendelea vizuri na ameanza kutoa sauti.


 

Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com