TANGAZO

TANGAZO

RAIS SAMIA ASHIRIKI MKUTANO WA PAMOJA WA WAKUU WA NCHI NA SERIKALIWA JUMUIYA YA EAC NA SADC KWA NJIA YA MTANDAO


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano wa Pamoja wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika kwa njia ya mtandao usiku wa tarehe 24 Machi, 2025 Ikulu ndogo ya Mkanyageni, Chake Chake, mkoa wa Kusini Pemba.


Mkutano huu ni wa pili kufanyika baada ya ule wa kwanza uliofanyika tarehe 08 Februari, 2025 Ikulu, Jijini Dar es Salaam na ulihudhuriwa na Wakuu wa Nchi na Serikali wafuatao:-

Rais William Ruto wa Kenya, Dkt. Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe, Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini, Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Paul Kagame wa Rwanda, Rais Lazarus Chakwera wa Malawi, Rais Andry Rajoelina wa Madagascar, Rais Hakainde Hichilema wa Zambia, Dkt. Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Waziri Mkuu wa Somalia pamoja na Mawaziri kutoka Sudani Kusini na Angola.






Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com