Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Machi 06, 2025 ni mgeni rasmi katika Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Kanda ya Kusini, yanayofanyika katika viwanja vya Maegesho, Nachingwea mkoani Lindi.
Kaulimbiu ya kongamano hilo kwenye Kanda ya Kusini ni: Ushiriki na Mchango wa Wanawake katika Kukuza Maadili, Uzalishaji na Kuongeza Mnyororo wa Thamani ya Mazao.