TANGAZO

TANGAZO

RAIS SAMIA APEWA TUZO YA MAGEUZI KATIKA MISITU, UHIFADHI

 



Na Mwandishi Wetu, Njombe


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amepewa tuzo ya Wizara ya Maliasili na Utalii kutambua mchango wake katika masuala ya uhifadhi wa misitu, mazingira na nishati safi.

Tuzo hiyo iliyokabidhiwa kwa niaba yake kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, imetolewa na Wizara hiyo kupitia kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Pindi Chana, mjini Njombe wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Misitu Duniani na Siku ya Kitaifa ya Upandaji Miti. 


Maadhimisho hayo ya kitaifa ambayo yamehudhuriwa na maelefu ya wananchi na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka, Naibu Waziri wa Utalii, Dunstan Kitandula, Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abbasi yameshuhudia pia maonesho ya teknolojia na bidhaa mbalimbali za misitu na utalii.






Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com