TANGAZO

TANGAZO

CHAKULA CHA ASKARI SIKU ZOTE NI MAZOEZI

 


Vyombo vya Ulinzi na Usalama Mkoani Songwe vyaungana na kufanya mazoezi ya pamoja ili kujenga umoja na kuendelea kuimarisha usalama Mkoani hapa.


Kauli hiyo ilitolewa Aprili 26, 2025 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Augustino Senga akizungumza kwa niaba ya vyombo hivyo alisema mazoezi haya ni muhimu kwa kila askari kwa ajili ya majukumu yake ya kila siku.


Kamanda Senga aliongeza kwa kusema mazoezi hayo ni sehemu ya kawaida ya utendaji kazi wao, ukiwa na lengo la kuhakikisha kuwa vyombo hivyo vinakuwa na utayari muda wote kitendo kitakachofanya Mkoa wa Songwe kuendelea kuwa salama.


Vilevile Kamanda Senga alisema kuwa wananchi wasiwe na wasiwasi kwani vyombo vyao vya dola vipo macho muda wote na vinaendelea kutekeleza jukumu mama la kulinda raia na mali zao pamoja na nchi kiujumla.


Kwa kuhitimisha, Kamanda Senga alitoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Songwe kuendelea kushirikiana na vyombo hivyo kwa kutoa taarifa za viashiria vya uvunjifu wa amani ikiwa ni pamoja na uhalifu na wahalifu ili viweze kushughulikiwa haraka na Mkoa wa Songwe uendelee kuwa salama

.





Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com