TANGAZO

TANGAZO

KATIBU WA CHADEMA NYASA ATIMKIA CCM




Aliyekuwa Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Wilaya ya Nyasa, Ndugu Jacob Benworth Kunani Leo Aprili 25, 2025 amejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Hafla fupi ya kumpokea iliyofanyika katika Ofisi za Umoja wa Vijana UV-CCM Wilaya ya Nyasa.

Akikabidhi Kadi ya CHADEMA Na kupokea Kadi ya CCM Kunani amesema anayofuraha kubwa kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kupokelewa na Viongozi wa UV-CCM Wilaya ya Nyasa na kusema kuwa amepata amani ya roho, kwa kuwa Chama cha Mapinduzi ni chama imara kinachoendeshwa kwa misingi ya amani na Utulivu na kipo kwa ajili ya kujenga Taifa na kuleta Maendeleo ndani na nje ya Tanzania
.


Ameongeza kuwa amejikuta ametoka kifungoni na sasa yuko huru, hata hivyo ameahidi kuwa atashirikiana vema na wanachama wa CCM.

 Mgeni Rasmi katika Hafla hiyo ni Komred Clavian Matembo mwenyekiti wa Umoja waVijana UV-CCM Wilaya ya Nyasa amempokea na kumkaribisha CCM na kumtaka awe mwanachama mwaminifu na kumsajili katika Mfumo wa Teknolojia ya Habari na mawasiliano ili mawze kupata kadi ya CCM pamoja na kumpa Tisheti ya Chama Cha Mapinduzi.



Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com