TANGAZO

TANGAZO

PICHA: UVCCM MTWARA WAFANYA TAMBIKO LA KIMILA KUMUOMBEA RAIS DKT. SAMIA


Katika mwendelezo wa kampeni ya Vijana wa Umoja wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mtwara ya “AMKA TWENDE NA SAMIA 2025”, Umoja wa Chama hicho wamefanya tambiko maalum kwa kushirikiana na wazee wa kimila wa mkoa huo, kumuombea Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan afya njema, ulinzi na baraka katika safari yake ya kuiongoza Tanzania.


Wamefanya tambiko hilo leo, Machi 6, 2025, Tambiko hilo limeambatana na maandalizi ya ziara yao kubwa ya mkoa mzima, inayolenga kuwaamsha vijana, kuhamasisha maendeleo na kuhakikisha kura za kishindo kwa Mhe. Rais katika uchaguzi wa mwaka 2025.


Sauti ya vijana wa Mtwara ni moja: “Tumeshuhudia kazi – sasa ni zamu yetu kulinda ushindi. Samia ni Tumaini la Taifa!”




Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com