Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi alipokuwa akiwasili katika Ukumbi wa Parokia ya Familia Takatifu Bombambili, Jimbo kuu Katoliki kwa ajili ya kufungua mkutano Mkuu Maalum wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), unaofanyika Songea mkoani Ruvuma.
Mkutano huo unafanyika leo April 04, 2025, umebeba Ajenda ya Uchaguzi wa ndani ya TEF kwa Nafasi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti pamoja na Wajumbe 7 wa Kamati ya Utendaji.