TANGAZO

TANGAZO

TAASISI YA MAMA 'MAMA ONGEA NA MWANAO' KUSHIRIKI MTOKO WA PASAKA


Na.  Mwandishi wetu - Dar es Salaam

Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao imesema itashiriki kikamilifu katika maandalizi ya Mtoko wa Pasaka utakaofanyika Aprili 20,2025 katika Ukumbi wa The Superdome Masaki Jijini Dar es Salaam ambapo lengo kuu ni kuwakutanisha watanzania kufurahia kupitia Nyimbo,Maombi na kutoa msaada kwa wakina Mama Wajawazito.


Hayo yamebainishwa na leo Aprili 7,2025 jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Steven Nyerere wakati akizungumza na Wanahabari amesema tukio hilo litakuwa la kiroho na kihistoria kwani litaliombea Taifa pamoja na kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan katika mwaka huu wa uchaguzi Mkuu.

Aidha ameeleza kwamba mambo yatakayolipamba tukio Hilo ni maonesho ya muziki wa Injili,yatakayoongozwa na mwanamuziki mashuhuri Christina Shusho ambaye ni mwanachama wa Taasisi hiyo,Shusho atapanda jukwaani pamoja na wanamuziki wengine kutoka ndani na nje ya nchi ya Tanzania


"Mtoko huu utakuwa wa kipekee sana ni mwaka wa tatu kushiriki,Nia na madhumuni ni kuwaunganisha watanzania na Afrika Mashariki katika amani na mshikamano na kuwaombea Viongozi wa Taifa",amesema Shusho.


Hata hivyo amesisitiza kwamba maombi na mshikamano ni njia ya kulinda amani ya Nchi huku kauli Mbiu ya Mwaka huu ikiwa ni :"Kwa Maombi Utashinda",

Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com