Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) akisikiliza maelezo kuhusu shughuli za uhifadhi, Utalii na utafiti alipotembelea banda la Wizara ya Maliasili na Utalii baada ya kufungua mkutano wa 73 wa Baraza la Viwanja vya Ndege Afrika unaofanyika Jijini Arusha, Maelezo katika banda hilo yametolewa na Kamishna MsaidizI Mwandamizi- Huduma za Utalii na Masoko NCAA Mariam Kobelo (aliyeshika Mic).
Wizara ya Maliasili na Utalii na taasisi zake imeshiriki katika Mkutano huo muhimu kutokana na mchango wa moja kwa moja kwenye Sekta ya Anga katika kusafirisha watalii wa ndani na nje kwenda kwenye maeneo yenye vivutio vya utalii nchini.