Msanii wa Muziki Bongo, Beka Flavour amedai haweza kujihushisha na timu yoyote katika muziki huo ili kunufaika na mashabiki wa timu fulani kwani yeye anatengenezea kazi nzuri ambazo anajua zinaweza kupendwa na wote.
Beka Flavour amesema anafanya muziki mzuri kwa ajili ya mashabiki wake ambao wapo naye kwa ajili ya ubora wa kazi zao na sio timu ambazo kamwe hawezi kujiunga nazo.
"Utimu kweli unachangia kuua muziki lakini mimi kwenye hilo siwezi kusema kwa sababu sina timu, yaani mimi mwenyewe sina timu yangu (timu Beka). Sitoruhusu kuwa kwenye timu ya aina yoyote, mtu ambaye anapenda muziki wangu, atanisapoti, mtu ambaye anasapoti kwa ajili ya muziki wa timu hiyo basi awe nao tu, nachohakikisha naimba muziki mzuri ambao kila mtu ataupenda," amesema.
"Lakini hao wenye timu zao kuna vitu vinawafaidisha, kama vina manufaa, basi waendelee kuvifanya lakini kwa upande chanya, wasifanye kwa mambo mabaya kwa sababu zikizidi sana watu wanaweza kuuana au kupigana," amesema Beka.
Kwa miaka ya hivi karibuni wasanii Alikiba na Diamond Platnumz wamekuwa ni washindani wakubwa ambao wametengeneza timu ambazo hadi baadhi ya wasanii wengine wamejiunga nao.