TANGAZO

TANGAZO

SPIKA TULIA ASHIRIKI IBADA YA MAZISHI YA ALIYEKUWA ASKOFU MKUU WA KWANZA WA KANISA LA TAG


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ameshiriki ibada ya mazishi ya aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kwanza wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Askofu Immanuel Lazaro. Ibada hiyo imefanyika leo, tarehe 27 Mei 2025, katika Kanisa la TAG – Jerusalemu Mudio, lililopo Kata ya Masama, Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro.


Askofu Immanuel Lazaro alifariki dunia tarehe 17 Mei 2025 katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC), ambapo alikuwa akipatiwa matibabu.






Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com