TANGAZO

TANGAZO

WANANCHI WAASWA KUACHA TABIA YA KUJITIBU NYUMBANI

 


Wananchi Wilaya ya Babati wameaswa kuacha tabia ya kujitibu nyumbani pindi wanapojihisi kuumwa na badala yake kwenda vituo vya kutolea huduma za afya kwa ushauri na vipimo zaidi.


Wito huo umetolewa Wilayani Babati Mkoani Manyara na Mfamasia Mwandamizi kutoka Baraza la Famasi Tanzania Bi. Anna Tema wakati akitoa Elimu ya Afya kuhusu matumizi sahihi ya dawa kwa Wananchi waliohudhuria kupata huduma za Afya katika Hospitali ya Mji wa Babati ikiwa ni mwendelezo wa Baraza la Famasi wa utoaji wa Elimu ya Afya kwa jamii kwa kushirikiana na Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma.


”Tuache kujitibu nyumbani,tuache kutumia dawa kiholela, kwa sababu inaleta athari kwenye afya zetu"amesema.


Akiwa katika soko Kuu la Babati ameishauri jamii kupima kwanza na kupata ushauri wa daktari kabla ya kutumia dawa.


Kwa upande wake Erick Bokango kutoka Baraza hilo amesema ni muhimu kufuata maelekezo sahihi ya wataalamu wa afya katika kulinda afya bora.


Simon Gadiye ni Mfamasia wa Halmashauri ya Mji wa Babati ametoa wito kwa jamii kuacha tabia ya kununua holela dawa kwa maduka yasiyosajiliwa na Baraza la Famasi Tanzania.

"Niwasihi wananchi kuacha kununua dawa kwa maduka yasiyosajiliwa kwani ukipata tatizo unashinda uanzie wapi kufuatilia wapi?amesema.

Nao baadhi ya wananchi wa Babati akiwemo Babu Majoka ameishukuru Serikali kupitia Baraza la Famasi Tanzania na Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma kwa kuendelea kutoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya dawa.

"Nashukuru nimepata elimu ya afya, haya maelekezo nitayazingatia, tusikimbilie kununua dawa bila kupima "amesema.

Ikumbukwe kwa Baraza la Famasi Tanzania kwa kushirikiana na Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma limeendelea na Kampeni Maalum ya utoaji wa Elimu ya Afya katika Mikoa ya Pwani, Morogoro,Singida,Manyara, Kilimanjaro na Tanga.

Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com