Ikumbukwe kuwa mradi wa SGR ni mojawapo ya miradi mikubwa ambayo iliwapa wasiwasi wananchi alipofariki Rais wa awamu ya Tano Dkt. Magufuli, wakiamini kuwa aliyekuwa makamu wake pengine hataweza kuiendeleza na kuikamilisha.
Hata hivyo Dkt. Samia aliweza na alikwenda mbali zaidi kwa kuanzisha miradi mingine mikubwa ya SGR. Haishangazi kuona leo akitumia SGR kufika katika mkoa wa Morogoro. Katika moja ya nukuu leo akiwa jukwaani Morogoro mjini Dkt. Samia aliwambia wananchi na wafuasi waliokuwa wanamsikiliza kuwa
“Ndugu zangu wa Morogoro, leo safari yangu ya kuja Morogoro ilikuwa nyepesi sana, nimetumia reli ya SGR, niliondoka Dar es salaam majira ya saa nne, saa tano nilikuwa Ngerengere na, saa sita nipo Morogoro’’.