TANGAZO

TANGAZO

VITONGOJI VYOTE KUWAKA UMEME 2025- 2030


Mgombea wa Urais kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameahidi wananchi wa mkoa wa Morogoro kuwa endapo watamchagua katika uchaguzi mkuu kufikisha umeme katika vitongoji vyote vilivyosalia katika mkoa wa Morogoro. 

Katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake vijiji na mitaa yote ya mkoa wa Morogoro vimefikishiwa huduma za umeme sambamba na vitongoji vingi. 

Kwa mujibu wa takwimu katika kpindi cha uongozi wa miaka minne ya uongozi wake vijiji vilivyofikishiwa huduma ya umeme vimeongezeka kutoka vijiji 437 mwaka 2020 hadi 659 mwaka 2025. Hali ya upatikanaji wa umeme ilikuwa chini asilimia 46 mwaka 2020 ila sasa hali ya upatikanaji wa umeme ni zaidi ya asilimia 90 mwaka 2025. 

Dkt. Samia ameahidi kuwezesha ongezeko la upatikanaji wa umeme ili kuwezesha matumizi ya nishati safi katika ngazi ya kaya, sambamba na hili ameongeza kuwa serikali atakayoiunda itajenga vituo vya kupooza umeme katika mkoa wa Morogoro. 

Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com