Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWACHA) Kanda ya Serengeti Ndugu Resemary Kiligini ambaye amewahi pia kuwa Mbunge (CCM) na Mkuu wa Wilaya za Meatu na Maswa amejiunga na ACT Wazalendo katika mkutano wa mapokezi ya mgombea Urais wa ACT Wazalendo Ndugu Luhaga Mpina yaliyofanyika Jimbo la Kisesa leo tarehe 16 Agosti 2025.

