Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Professa Kitila Mkumbo leo Agosti 27, 2025 amerudisha fomu yake ya uteuzi wa kugombea kwenye jimbo hilo ili kuteuliwa na Tume Huru ya Uchaguzi(INEC).
Kitila ambaye amekuwa Mbunge wa jimbo hilo kuanzia mwaka 2020 leo amerejesha fomu baada ya kuichukua Agosti 25 na kukamilisha kuijaza.
Kitila akiambatana na mgombea Ubunge wa Jimbo la Kibamba(CCM), Angellah Kairuki walisindikizwa na mamia ya wanachama wa CCM, madereva pikipiki(bodaboda), bajaji na wafanyabiashara wadogo wa vyakula(Mama ntilie) kuanzia Ofisi za CCM jimbo la Ubungo mpaka jirani na zilipo ofisi za Msimamizi wa Uchaguzi.