Hii ni sawa na ongezeko la hospitali 52, vituo
vya afya 300 na zahanati1,000.
Vilevile, upatikanaji wa dawa na vifaa tiba
umeongezeka kutoka wastani wa asilimia 92
mwaka 2020 hadi asilimia 95 mwaka 2025,
tofauti ya alama 3 za asilimia.
Ongezeko hili limetokana na kuongezwa kwa bajeti ya sekta ya afya, maboresho ya Bohari ya Dawa na mkakati wa Serikali kuhakikisha huduma za afya zinapatikana karibu na wananchi.

