Serikali ya Awamu ya Awamu ya Sita Chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imelipa madeni mengi ya wakandarasi yenye jumla ya shilingi Trilioni 1.01.
Serikali imeendelea kulipa madeni yaliyohakikiwa ambapo kiasi cha shilingi trilioni 1.01 kimelipwa.
Ulipaji wa madeni haya umesaidia kulinda mitaji na kuchochea shughuli za kiuchumi nchini kwa kuwezesha wakandarasi, wazabuni na watoa huduma kuendeleza miradi, kulipa wafanyakazi wao,na kuwekeza katika shughuli mpya za uzalishaji.
Hatua hiyo pia imeimarisha uaminifu wa Serikali mbele ya wadau wa ndani na nje ya nchi, kupunguza mzigo wa madeni yasiyolipwa, na kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayochangia ukuaji wa uchumi na ustawi wa wananchi.
