Chini ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, idadi ya wanafunzi wa shule za awali imeongezeka kutoka 1,278,886 hadi 1,558,549, ongezeko la 21.87%, huku shule zenye madarasa ya awali zikiongezeka kutoka 16,355 hadi 18,011.
Ruzuku ya Elimu bila Ada imeongezeka kutoka Shilingi bilioni 249.66 hadi 484.27, ongezeko la 93.97%, Hii imerahisisha vijana wenye sifa kuendelea na masomo bila kizuizi cha kifedha.
Aidha, uandikishaji wa wanafunzi wenye mahitaji maalum umeongezeka kutoka 28,482 hadi 78,429, ongezeko la 175%.


