Chini ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan,uimarishaji wa huduma za afya na utoaji wa huduma za M-koba umeongeza idadi ya akina mama kuhudhuria kliniki.
Mahudhurio ya akina mama wajawazito kwenda kliniki yameongezeka kutoka 2,374,666 mwaka 2020 hadi 3,143,332 mwaka 2024, ongezeko la 768,666 au asilimia 32.3.
Aidha, idadi ya wajawazito waliohudhuria kliniki kwa mara ya kwanza kabla ya wiki ya 12 imeongezeka kutoka 848,149 mwaka 2020 hadi 1,186,812 mwaka 2024, ongezeko la 338,663 au asilimia 39.9.
Hii yote imechochewa na uimarishaji wa huduma za afya kwa kina mama ambao umefanyika ndani ya miaka minne.
