Chini ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, shule zenye kufundisha masomo ya Sayansi ya Fizikia, Kemia, Baiolojia na Hisabati zimeongezeka, huku idadi ya wanafunzi wanaosoma masomo haya katika shule hizo za sekondari kuanzia kidato cha tatu ikiongezeka kutoka 2,497,450 hadi 2,792,584, ongezeko la 295,134.
Aidha, ujifunzaji na ufundishaji wa stadi za kazi na lugha, ikiwemo lugha za alama katika elimu ya msingi, imeongezeka kwa kuajiri walimu 127 wa lugha za alama na kusambazwa katika shule 127.
Pia, shule 28 za mchepuo wa elimu ya ufundi/amali zimekarabatiwa na kupewa vifaa vya kisasa, huku shule 274 za michepuo ya kilimo na 28 za michepuo ya biashara pia zikiboreshwa.
