Chini ya Rais Samia, ujenzi na ukarabati wa Kivuko cha MV TANGA katika Mto Pangani, Mkoa wa Tanga kimegharimu jumla ya shilingi 1,118,092,480/= sawa na takriban dola za Marekani 450,000. Kivuko hiki kina uwezo wa kuvusha watu 100, magari 6 na mizigo yenye uzito wa jumla ya tani 50 kwa pamoja.
Ujenzi wa kivuko hiki utarahisisha mawasiliano kati ya Pangani Kaskazini na Pangani Kusini, na inakisiwa kutazalisha jumla ya ajira 70, ambazo za moja kwa moja ni 30 na zisizo za moja kwa moja ni 40.
Lengo la Rais Samia ni kukuza uchumi wa buluu, kurahisisha usafiri na kuharakisha maendeleo kwa wananchi wake.