TANGAZO

TANGAZO

MAJALIWA MGENI RASMI MKUTANO WA WADAU WA LISHE



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Septemba 30, 2025 ni mgeni rasmi katika mkutano wa kumi na moja wa wadau wa lishe unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa APC uliyopo Bunju jijini Dar es Salaam



Mkutano huo ni jukwaa linalounganisha wadau wote wa lishe kujadili hatua zilizofikiwa, changamoto zilizopo na namna bora ya kuimarisha jitihada za pamoja katika kupambana na utapiamlo na kukuza afya za watanzania.



Pia, Mkutano huo unalenga kujadili na kuimarisha utekelezaji wa Mpango Jumuishi wa Pili wa Kitaifa wa Lishe (2021/22-2025/26)

Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com