TANGAZO

TANGAZO

CHINI YA UONGOZI WA RAIS SAMIA VIWANDA VYA SUKARI VYAIMARISHWA NA KUBORESHWA

 


Chini ya Rais Samia Serikali imeendelea na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Kiwanda cha Sukari Mkulazi kwa kuhakikisha kuwa kiwanda kinafanya kazi kikamilifu, kinatoa ajira na kinachangia katika uchumi wa taifa. Aidha uzalishaji wa sukari ulianza mwezi Julai, 2024, na kimezalisha tani 19,124 za sukari ya majumbani vile vile kimetoa ajira za moja kwa moja 2,172 na zisizo za moja kwa moja 8,000. 

Kwa mujibu wa hotuba ya bajeti ya wizara ya viwanda na biashara ya mwaka 2025/26; Serikali pia imefanya upanuzi unaohusisha usimikaji wa mitambo yenye uwezo mkubwa wa kuzalisha sukari na inayotumia teknolojia ya kisasa katika kiwanda cha Sukari cha Kilombero na Kiwanda cha Sukari cha Kagera. 

Katika Kiwanda cha Kilombero upanuzi unatarajiwa kuongeza uzalishaji wa 80 sukari kutoka tani 132,000 za sasa hadi tani 271,000 za sukari ifikapo mwaka 2025/2026 na kutoa ajira 4,634. 

Aidha, upanuzi huo utagharimu zaidi ya shilingi bilioni 570 hadi utakapokamilika. Hadi kufikia Machi, 2025 upanuzi umefikia asilimia 98 ambapo majaribio ya kuendesha mitambo yanaendelea. 

Kwa upande wa kiwanda cha Kagera, upanuzi unatarajiwa kuongeza uzalishaji wa sukari kutoka tani 131,000 kwa sasa hadi tani 170,000 za sukari ifikapo mwaka 2025/2026.

Kiwanda hicho kimetoa ajira za moja kwa moja 10,500 na ajira zisizo za moja kwa moja 60,000. Juhudi hizi zimeendelea kuimarisha hali ya upatikanaji sukari nchini. 

Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com