TANGAZO

TANGAZO

DKT. SAMIA AWAOMBA WANANCHI WA UVINZA KUMCHAGUA ILI KUENDELEA KUIMARISHA SEKTA YA AFYA


Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, siku ya jana tarehe 13 Septemba 2025 aliendelea na mikutano ya kampeni katika wilaya ya Uvinza ambapo alipokelewa kwa shangwe na maelfu ya wananchi, viongozi wa dini, wazee wa kimila, viongozi wa chama, wagombea ubunge na madiwani pamoja na wanahabari.



Akiwa pale, alishukuru Mwenyezi Mungu kwa nafasi ya kuanza kampeni zake Kigoma katika wilaya ya Uvinza na kwa mapokezi ya heshima na upendo aliyopewa. 

Dkt. Samia alianza kwa kukumbusha kuwa mwaka 2020 CCM iliinadi ilani yake na katika kipindi cha miaka mitano utekelezaji wake umefanyika kwa kiwango kikubwa, hivyo serikali yake inapata ujasiri wa kuomba tena ridhaa ya wananchi. 

AFYA 

Mgombea wa Urais kupitia CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan aliwaomba wananchi wa Uvinza kumchagua katika uchaguzi mkuu ujao ili kuendelea kuimarisha sekta ya afya, ambapo alitanabainisha mafanikio makubwa yaliyopatikana, ikiwemo, Ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Uvinza, Kuongezeka kwa vituo vya afya na ujenzi wa zahanati nyingi na Upatikanaji wa dawa kuongezeka kutoka 11% na kufikia asilimia 91. 

Aidha, alisema kuwa serikali ya CCM itakapopewa ridhaa katika uchaguzi mkuu ujao itaanza majaribio ya utekelezaji wa mpango wa Bima ya Afya kwa Wote, kabla ya kuupanua kitaifa. Pia, Aliahidi kujenga vituo vya afya vya Kadanga, Kabeba na Kasanza, kukamilisha zahanati za Msihezi, Lagosa, Sambala, Lulinga na Kahwibili, pamoja na kukamilisha jengo la mama na mtoto Liabusende na kituo cha afya Kazuramimba. 

ELIMU 

Dkt. Samia Suluhu Hassan amebainisha kuwa serikali yake imetumia zaidi ya shilingi bilioni 13 kuboresha shule za msingi 34, jambo lililosaidia kukidhi mahitaji ya udahili. Pia shilingi bilioni 19 zimetumika kujenga shule za sekondari hadi kufikia 31, na shilingi bilioni 2.8 kukamilisha ujenzi wa VETA. 

Hii imeimarisha mazingira bora ya kujifunza na kuendeleza elimu bila ada. Dkt Samia ameahidi kuwa baada ya haya mafanikio hatua inayofuata ni kukamilisha kituo cha walimu Uvinza.

 KILIMO NA MASOKO 

Akizungumzia sekta ya kilimo, Dkt. Samia alisema wakulima wa Uvinza, hasa kina mama, wamefaidika na ruzuku ya mbolea na pembejeo pamoja na huduma za ugani. Serikali itaendeleza utoaji wa ruzuku na huduma hizo. 

Aidha, akitambua changamoto ya soko, aliahidi kujenga soko kubwa ili kina mama wauze bidhaa zao kwa urahisi na faida. NISHATI Kuhusu sekta ya nishati Dkt. Samia amesema wilaya nzima ya Uvinza imeunganishwa na umeme, na kazi inayoendelea sasa ni kufikisha huduma hiyo kwenye vitongoji vyote. Kaya zenye umeme zimeongezeka kutoka 2,072 mwaka 2020 hadi 9,613 sasa. 

Alisisitiza kuwa umeme huu utachochea viwanda vidogo vya kuongeza thamani ya mazao. 

UVUVI NA UWEKEZAJI 

Sekta ya uvuvi pia imepewa kipaumbele. Serikali imeleta shilingi milioni 442 kwa mikopo ya riba nafuu kwa wavuvi na vijana, sambamba na fursa kubwa za mradi wa reli ya kisasa (SGR) unaopita Uvinza kuelekea 

Msongati nchini Burundi. Alieleza kuwa reli hiyo itafungua fursa kubwa za biashara na ajira. 


Kama una Taarifa,Picha, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kwa simu +255 766 166 125 au Email : emmymwaipopo@gmail.com