Balozi wa Tanzania nchini Comoro Saidi Yakub ameipongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kupeleka idadi kubwa ya madaktari bingwa bobezi katika kambi ya matibabu nchini humo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, alilolitoa wakati wa ziara yake visiwani humo.
Akizungumza hii leo katika mahojiano maalumu na Afisa Habari kutoka Idara ya Habari ya MNH, Balozi Yakub amesema hospitali hiyo imepeleka jumla ya madaktari bingwa saba wa mgonjwa mbalimbali ukilinganisha na taasisi nyingine zinazoshiriki kambi hiyo.
"Hospitali ya Muhimbili imetuletea zaidi ya madaktari saba na katika wataalam hao watakuwa katika mgonjwa ya figo, ngozi, macho, meno, masuala ya uzazi kwa akina mama pamoja na magonjwa ya kinamama"
Aidha, Balozi Yakub ameongeza kuwa licha ya kambi ya matibabu kuanza kuanza Oktoba 04, 2025, tayari zaidi ya watu 1000 wamekwisha kujisajili ili kupata huduma za kibingwa na ubingwa bobezi.